https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Pambo&oldid=1107387
https://sw.wikipedia.org/w/index.php?title=Pambo&oldid=1107387
SW.WIKIPEDIA.ORG
Pambo
Pambo (wingi: Mapambo kutoka kitenzi: kupamba) ni kitu au kifaa kinachotumika kuongezea urembo au uzuri wa mtu, nyumba, au kitu kingine chochote. Tangu zamani za kale binadamu ameonyesha kipaji chake cha usanii kwa kupamba vitu mbalimbali, hasa vile vinavyomhusu zaidi, kama vile mavazi yake na mwili wake mwenyewe. Mapambo katika ujenzi Katika ujenzi na sanaa ya mapambo ni zana zinazotumika kutia nakshi eneo au kitu fulani. Mapambo kwa ajili ya majengo huchongwa kutoka kwenye mawe, mbao au vito vya thamani, udongo, au pia mengine huchorwa juu yake, k.mf. juu ya kitambaa. Mitindo mbalimbali ya mapambo imegunduliwa kupitia sanaa na ujenzi, ikiwemo ya ufinyanzi, samani na kazi za uhunzi pia. Kwenye nguo, kuta na vitu vingine ambapo mapambo yaweza kuwa kitu pekee kinachosaidia kuwepo kwake, michoro na miundo pia hutumika zaidi. Miundo mbalimbali inayotumika katika michoro ya mapambo hutolewa katika maumbo ya kijiometri, na maumbo ya maua, picha, michoro mbalimbali kama ya mimea na wanyama pia. Aina za mapambo anayovalia binadamu ...
5 Tags 0 Shares 1 Views

Password Copied!

Please Wait....