https://sw.wikipedia.org/wiki/Maandishi
https://sw.wikipedia.org/wiki/Maandishi
SW.WIKIPEDIA.ORG
Maandishi
Maandishi (pia: mwandiko) ni tendo la kushika sauti za lugha kwa njia ya alama zinazoandikwa. Mitindo ya miandiko Sehemu kubwa ya maandishi duniani inatumia alfabeti mbalimbali. Kati yake alfabeti ya Kilatini imesambaa zaidi, ikifuatwa na alfabeti ya Kiarabu na alfabeti ya Kikirili. Asia ya Mashariki imeendelea kutumia maandishi yake ya alama zinazodokeza neno lote badala ya herufi tu. Mtindo wa kutumia alama kwa neno lote ulitumiwa pia katika utamaduni wa Misri ya Kale na Meksiko ya Kale. Miandiko ya Uhindi, inayotokana na mwandiko wa Brahmi, hutumia miandiko mbalimbali inayoonyesha silabi. Hata lugha za Ethiopia hufuata mtindo wa kufanana nayo. Historia ya maandishi Hakuna hakika maandishi yalianza lini na wapi. Wataalamu wengi huona ya kwamba Sumer katika Mesopotamia ilikuwa na maandishi ya kwanza duniani. Wengine huona ya kwamba sanaa ya kuandika ilianzishwa na watu mbalimbali kwa nyakati tofauti katika pande mbalimbali za dunia. Si rahisi kuwa na hakika kwa sababu maandishi yenyewe hudumu kwa muda tu kutegemeana na mata na vifaa vilivyotumiwa. Maandishi...
11 Tags 0 aandelen 1 Views

Password Copied!

Please Wait....